Friday 8 November 2013

CHEKA KIDOGO: KAZI YA KUFUNGUA


Mchungaji alikuwa kanisani akihubiri. Mwanzoni kabisa wa mahubiri alisema: “Siku ya leo ni njema kabisa machoni pa Bwana, kwa sababu leo tunakwenda kufungua vifungo vyote vya sheti. Kwa hiyo, tutafumba macho na kila mmoja aanze kuomba, afungue kila kitu kinachomkwaza… Naamini Bwana atasikia na maombi yako yatajibiwa. Haya, tufumbe macho sasa tuombe…”
Baada ya hapo kila mtu akapaza sauti yake kuomba kwa kila hitaji lake. Mchungaji aliposema ‘AMEN’ na watu wote wakaitikia na kufumbua macho.
Mara ikasikika sauti kutoka katikati ya waumini: “Bwana asifiwe, nimeweza!” Binti mmoja akainuka akishangilia huku kifua chake kikiwa wazi. Kabla hajaulizwa kulikoni huku wengine wakishangilia, yeye akasema: “Mwezi sasa nahangaika na sidiria hii, nimejaribu kuifungua imeshindikana, mpenzi wangu naye amehangaika kuifungua imeshindikana. Lakini leo imefunguka…!”
Wakati huyo akieleza, kijana mwingine naye akainuka na kusema: “Hata mimi imefunguka…!”
Wenzake wakamuuliza: “Nini?” maana hawakumuona akihangaika sana.
Akajibu: “Zipu! Ni baada ya kuyaona matiti ya huyo dada…”

No comments:

Post a Comment