Thursday, 24 October 2013

KWANINI UNAWAZA NGONO TU, KILA WAKATI

Mwanamuziki George Michael

Na Brother Danny

IWE ni utumwa au ni shurutisho, lakini baadhi ya watu hawawezi kuacha kufanya mapenzi na mara nyingi huwa wanatambua kwamba wana matatizo mara baada ya kitendo chenyewe, na hapo ndipo Waswahili husema; "Kijuto msuto kisicho kito!" Hujutia kitendo hicho wakati wameshakifanya.
Wakati mwanamuziki mkongwe wa miondoko laini wa Marekani, George Michael, alipokamatwa mnamo Aprili 7, 1998 akikabiliwa na shtaka la kulawitiwa kwenye choo cha mbuga ya wanyama huko Beverly Hills, magazeti mengi yaliandika yalivyojua. Gazeti la New York Post la Aprili 9, 1998 liliandika kwa maandishi makubwa ukurasa wa mbele DOWN & OUTED IN BEVERLY HILLS na tangazo lililokuwa ndani ya habari hiyo liliandika kidaku zaidi likisema ZIP ME UP BEFORE YOU GO GO, yaani 'Nifunge zipu kabla ya kuondoka!'. Habari nyingi za kidaku ziliandikwa, kila gazeti likiwa na kichwa tofauti cha habari kuelezea tukio hilo moja, na zaidi kwa sababu Michael siku zote alikuwa msiri kuhusu jinsia yake, akiwa hataki kutoa taarifa thabiti ya jinsia gani aliyokuwa akiipendelea kutokana na vitendo vya kishoga vilivyokuwa vikiripotiwa dhidi yake. Lakini mwanamuziki mwingine mkongwe Boy George ambaye pia ni shoga alimweleza Michael asione aibu. "We are sisters under the skin," yaani "Sisi ni wanawake ndani ya ngozi" aliandika katika barua ya wazi iliyochapishwa kwenye gazeti la The Express la London mara baada ya kukamatwa kwa Michael.
Mshtuko hata hivyo haukuwa mkubwa eti kwa sababu Michael alikuwa shoga. Tetesi kuhusu ushoga wa George Michael zilikuwa zimesambaa kwa miaka kadhaa na katika mahojiano mwaka 1997 alizungumzia kuhusu mapenzi yake kwa mwanamume mmoja wa Brazil aliyefariki kutokana na matatizo ya ubongo mwaka 1993. Kitu ambacho kila mmoja alikuwa akijiuliza kilikuwa, "Alikuwa kifanya nini bafuni?" Yeye ni mwanamume tajiri, mwenye kipaji na mvuto. Kama alikuwa akifanya kile ambacho alituhumiwa nacho, kama alikuwa akijaribu kufanya mapenzi na mtu katika chumba cha kupumzika watu wote, ni kwa nini akachagua choo kuwa ndiyo mahali muafaka pa kufanyia mapenzi? Watu wachache walishangaa kwa sauti, Hivi George Michael ni mtumwa wa ngono?
Wakati Michael alipozungumza kupitia kituo cha luninga cha CNN siku chache baada ya kukamatwa kwake, pia alimaanisha, bila kueleza kinaganaga, kwamba yeye ana tatizo. "Nadhani ni hatari ya hali yenyewe ndiyo iliyosababisha nikafanya vile, kwa sababu hakika ilikuwa kama shurutisho," Michael alimweleza mwandishi Jim Moret. Mapema katika mahojiano hayo Michael alikuwa amesema, "Siwezi kusema pia kwamba hiyo ilikuwa ndiyo mara ya kwanza kutokea. Unajua, nimejiweka katika nafasi hiyo kabla. Ninachoweza kufanya ni kuomba samahani tu. Ninaweza kujaribu kufikiria kwa nini nilifanya vile, kuielewa jinsia yangu kwa undani kidogo, lakini, bila kutarajia, upande wangu mmoja unaamini kwamba baadhi ya shurutisho hizi ni kwamba ningeweza kufumaniwa... Najiona mpumbavu na mzembe na dhaifu kwa kuruhusu jinsia na tamaa yangu ya mapenzi ikafichuka namna hii."
Wakati ni rahisi kujua nini kinachoendelea katika fikra za Michael, maneno yake yanafanana na yale yanayotumiwa na watumwa wengi wa ngono kuelezea baadhi ya vitendo vyao vibaya na namna walivyojisikia wakati walipofumaniwa.
Mwitikio kutokana na tukio la Michael ulizusha mdahalo wa mara kwa mara miongoni mwa mshoga na wasagaji kuhusiana na tafsiri tofauti za utumwa wa ngono na uhuru wa ngono. Kama ungezungumza na wataalamu na watu wanaotambua uraibu basi wangekwambia kwamba Michael ni mtumwa wa ngono. Kama ungezungumza na Keith Griffith, mmiliki wa tovuti ya Cruising for Sex, mtandao ambao ulielezea mbuga ya huko Beverly Hills kwamba ina "vyumba vingi vya wanawake, basi ungeiona hasira yake. "wali ambalo nategemea polisi wangeulizwa," alisema Griffith baada ya tukio hilo, "ni kwa nini wanapoteza fedha nyingi za kodi katika shughuli kama hii."
Griffith na mashoga wengine, kama wanachama wa Sex Panic!-kundi linalozungumzi mapenzi huru lililoanziishwa mwaka 1997- wanaona kwamba mapenzi kwenye umma ndilo suluhisho la karne kwa karne za ukomeshaji wa mapenzi. Lakini mashoga na wasagaji wengi wanasema kwamba mapenzi katika sehemu za umma ni tofauti na uraibu, na kwamba bafu na klabu za mapenzi, hasa zile za usiku ambako watu wanaweza kufanya mapenzi hadharani, hasa katika nchi zilizoendelea, hazistahili kupigwa marufuku kwa sababu kufanya hivyo ni uonevu.
Kama lilivyo wazo lenyewe, uraibu wa mapenzi uliingia na mzigo wa siasa. Matukio ya miaka ya 1960 na 190, wakati wanaume mashoga na wanawake wasagaji waipoanza kuibuka kwa mara ya kwanza katika idadi kubwa na wakati watu wengi walikuwa wakipiga vita mapinduzi ya mapenzi, yalisababisha kutoweka kwa maradhi mengine ya mapenzi kifikra kama, ushoga na nymphomania-kutoka kwenye 'biblia ya afya ya akili', ambacho ndicho kitabu cha Diagnostic & Statistical Manual of Mental Disorders, maarufu kama DSM. Matatizo mengine yaliyojitokeza kwa kuwa na nguvu kidogo za kufanya mapenzi au kutokuwa nazo kabisa, kama uhanithi (impotence) na mshindo usiokomaa (premature ejaculation), yaliongezwa. Lakini baadaye, kutokana na kuibuka kwa maradhi ya zinaa kama herpes, kaswende (syphilis) na baadaye UKIMWI, kulikuwa na mtazamo tofauti kuhusu mfumo wa maisha wa mapenzi huru na rahisi - mfumo wa maisha ambao mashoga na wasagaji waliamua kuutumia zaidi na kihistoria ndio wanaouona kama ni sehemu yao hasa. Watu walikuwa wakifanya mapenzi kwa kiwango kikubwa na mambo mengi mabaya yakawakumba.
"Katika miaka ya 1970 tabia za mapenzi hazikuwakilisha patholojia, yaani sayansi ya magonjwa," anasema mwanasosholojia John Gangnon wa State University of New York huko Stony Brook. "Lakini katika miaka ya 1990, kwa sababu ya maradhi ya UKIMWI, kuwa na idadi kubwa ya wapenzi (inachukuliwa) siyo vizuri. Hii kwangu naiona kama siyo sahihi."
Lakini bado, utumwa wa ngono umeendelea kushikilia kasi. Waathirika wa ngono hawaachi kufanya mapenzi; hawakomi kuyatafuta, hawakomi kufikiria wala kufanya chochote katika maisha yao ili tu kukidhi kiu yao.
"Mapenzi ndicho kitu pekee ambacho kilikuwa muhimu kwangu," anasema Ken, ambaye amekuwa akitibiwa uraibu wa ngono kwa miaka kumi. "Ilikua kama kujaribu kula sukari peke yake. Inaweza kujaza tumbo lako, lakini unashinda na njaa." Ataalamu wanasema kwamba, waathirika wataendelea na tabia zao hata pale wanapokabiliana na matatizo mengi, kama kupoteza familia zao, kazi, uhuru wao, kufumaniwa wakifanya mapenzi au wakipiga punyeto na hata kupoteza maisha yao. Hawawezi kujidhibiti na wanajiona wako dhaifu. "Nilikuwa nateseka kwa njaa," anasema Ken, "na nilikuwa katika hatari ya kujiua."
Kama nilivyosema hapo awali, sababu zinazochangia uraibu wa ngono ni nyingi sana, lakini kikubwa ninachotaka kusema ni kwamba, "Mapenzi ndicho kitu pekee wanachokitaka." Kwa mtu ambaye ameraibiwa katika mapenzi, kauli hii huwa ubeti maarufu vichwani mwao. Hatimaye huwa kama ukweli. Utumwa wa mapenzi ni nini na kwa nini baadhi ya wanaume na wanawake wanaraibiwa katika mapenzi? Tatizo hili linawezaje kujulikana na namna gani wale walioathirika wanavyoweza kusaidiwa?

Utumwa wa Kisaikolojia
Utumwa wa mapenzi ni uraibu wa kisaikolojia, matokeo ya matamanio yasiyofikiwa ya utotoni. Watoto ambao mahitaji yao hubakia ykiwa hayatambuliki wanaweza kurekebisha kwa kujifunza udhibiti matarajio yao. Utaratibu huu wa udhibiti unaweza kuchukua muundo wa mawazo mabaya kama, "Mahitaji yangu hayahesabiki," "Kuwa karibu kunaweza kuumiza " na "Nastahili kupendwa." Mawazo kama haya hayatoshelezi mahitaji ya utotoni, kuyaacha kutawafanya wakumbane nao baadaye maishani mwao. Kama watu wazima, wapenzi walioraibiwa huendelea kubakia tegemezi kwa wengine kuwahudumia, kuwalinda na kusuluhisha matatizo yao.
Walioraibiwa kimapenzi huwa wana matumaini ya ajabu na hofu zisizokwisha. Kuhofia kukataliwa, maumivu, kuhofia mambo wasiyoyazoea na kutokuwa na mani na uwezo wao - au hata haki zao - kuelezea mapenzi, husubiri, huomba na hutumainia mapenzi, pengine ndio uzoefu wao mdogo kabisa.
Kwa waathirika, mapenzi: Yanadhoofisha na yana tamaa; Yanafichwa; Yanaepuka madhara au mabadiliko; Hukosa urafiki wa ndani na wa kweli: Ni tegemezi na yana madhara; na Hutaka yule anayependwa ndiye aonyeshe upendo wa dhati.

Madhara ya Utumwa wa Mapenzi
Penzi ililoraibiwa limegubikwa na tamaa ya kuiona dnia yote kama iko kwa mpenzi mmoja tu. Ukuaji na maendeleo yao yakiwa yamehribiwa mapema katika maisha yao, wapenzi walioraibiwa hung'ang'ana katika utambulisho wa wapenzi wao. Kama mpenzi wake ana mali nyingi au ni maarufu, basi kila mahali atakapokuwa atapenda kujitambulisha kama sehemu ya huyo mpenzi wake. Nakumbuka dada mmoja mwandishi wa habari ambaye sipendi kumtaja jina, wakati uhusiano wake ulipokuwa katika hatua za awali na mchezaji mmoja wa klabu moja kongwe ya soka Tanzania, alikuwa akipenda kujitambulisha kama "Mama Fulani", yaani jina lake la ubini alikuwa akiliweka la yule mchezaji! Waandishi wenzake wengi, hasa wasichana wenzake, walikuwa wakimshangaa, akini yeye aliona fahari kubwa kujiita Mama Fulani. Huu ni utumwa wa mapenzi bila yeye mwenyewe kujijua. Watu wa namna hii hupenda kupata sifa kwa migongo ya wapenzi wao, na wakati mwingine watu hawa hupenda kulazimisha wapatiwe upendeleo fulani kutokana na umaarufu, utajiri au uwezo na mafankio ya mpenzi wake.
Kutokana na hofu ya mabadiliko, wapenzi walioraibiwa watatunisha maendeleo ya nafsi zao, wakitafuta ulinzi wakiamini kwamba hawawezi kutofautishwa kutoka kwa wapenzi wao. Wakati mwingine hofu ya mabadiliko ni kubwa kiasi kwamba maendeleo na uwezo binafsi, haja na tamaa zao nyingine huyeyuka.
Haja ya kuwa na ulinzi na utegemezi huleteleza matatizo ya kihisia. Wapenzi ambao ameraibiwa wanahadaika kwamba kufanya mambo kwa kuwafurahisha wapenzi wao kutawafanya wapendwe. Mfano kupendelea kumnunulia mpenzi wako zawadi, kadi a maua, na hata kumsifia kila wakati au kumgana kila mahali. Hali hii ni mbaya sana na watu wengi wamekuwa wakifanya hivi bila kutambua kwamba kuna madhara, na tena ni utumwa ambao mtu amejipa bila mwenyewe kutambua.
Kama utagundua kwamba uko katika uhusiano wa aina hii, unapaswa kutafuta msaada wa kitaalamu haraka sana, vinginevyo unaweza kuharibikiwa zaidi.
Tukutane wakati mwingine. Niandikie kupitia: brotherdanny5@gmail.com au +255 715 070 109

No comments:

Post a Comment