Mwalimu mmoja alikuwa anafundisha wanafunzi wa darasa la tatu somo kuhusu serikali, hivyo kazi ya ziada aliyowapa siku hiyo ni kwa wanafunzi hao kwenda kuwauliza wazazi wao serikali ni nini.
Samuel, aliyekuwa na miaka 7, alirudi nyumbani siku hiyo na kwenda kumuuliza baba yake serikali ni nini.
Baba yake akafikiria kwa muda kisha akamjibu: "Tazama kwa namna hii: Mimi ndiye rais, mama yako ni Bunge, huyu dada wa kazi ndiye nguvukazi, wewe ndio wananchi na mdogo wako Peter ndiyo maendeleo ya kesho."
"Baba, sijaelewa vizuri," Samuel akamuuliza baba yake.
"Kwa nini usiende kulala kwenye serikali? Pengine utaielewa vizuri," baba yake akajibu.
"Sawa... usiku mwema," Samuel akasema na kwenda kulala chumbani kwake pamoja na mdogo wake Peter (2).
Usiku wa manane Samuel akashtushwa na kilio cha mdogo wake. Akamtazama pale kitandani na kuona kwamba alikuwa amejiharibia (amejisaidia haja kubwa). Basi Samuel akaenda chumbani kwa wazazi wake ili wasaidie kumsafisha mdogo wake.
Akachungulia kupitia kwenye tundu la funguo na kumuona mama yake akiwa anakoroma, lakini baba yake hakuwepo. Akaenda kwenye chumba cha dada wa kazi. Alipochungulia kupitia kwenye tundu la ufunguo akamuona baba yake akifanya mapenzi na dada wa kazi. Samuel akashangaa, lakini akawa amepata picha ya swali lake na kufikiria huku akisema kwa sauti, "Ooh! Sasa naielewa vyema serikali! Rais anafanya mapenzi na nguvukazi, Bunge linakoroma, hakuna anayewajali wananchi, na maendeleo yametapakaa kinyesi!''
No comments:
Post a Comment