Thursday, 24 October 2013

KWANINI WATU WANAKUWA WATUMWA WA NGONO?


Na Brother Danny
JOHN alijiingiza katika tabia za utumwa wa ngono wa aina tatu: 1) kupiga punyeto kila wakati, 2) kutazama picha za ngono, na 3) majumba ya kufanyia massage. Alikuwa pia ni mlevi kupindukia. Kutokana na ushauri aliopewa na Joe Zychick, mtaalamu wa mambo ya saikolojia wa Marekani, alijifunza kwamba haijalishi kama alikuwa akinywa bia, mvinyo au pombe kali, iwe alikunywa nyumbani, baa, wakati wa wikiendi au wakati wowote. Alitakiwa kupambana na kuyashinda majaribu yote ya ulevi.
Tofauti na pombe - tabia za utumwa wa ngono haziko sawa. Watu wengi wanapambana na uraibu wa ngono kama vile ulevi kwa sababu, kwa nchi ya Marekani, Programu ya Hatua-12 ndiyo maarufu. Lakini kwa bahati nzuri kuna tiba ambayo ni nzuri zaidi. Ngoja tuangalie kwa undani na tupate tafsiri ya uraibu ambao unaweza kutumiwa kwenye ulevi na ngono kwa pamoja,  na uraibu mwingine: Uraibu ni "shughuli" au "kitu" ambacho mtu hukitumia "kuepuka" kupambana na mawazo au hisia "zisizoburudisha" ambazo zinapaswa kukabiliwa.
John alikuwa ameraibiwa na ulevi kwa sababu: badala ya kupambana na hali nzito ya kijamii, yeye alikunywa sana ili kupunguza fadhaa. Vijinasaba vyake havikumshawishi afanye hivyo, wala wazazi wake, wala jamii, au hata mpangilio mbovu wa kemikali. John aliamua kwa hiari yake kufanya hivyo. Badala ya kutafuta suluhu, yeye aliyasahau kwa kwenda kunywa pombe. Ulikuwa ni uamuzi wake. John alipokosa kujiamini katika mazingira fulani, alitumia kileo kwa kuyaondoa mawazo hayo kwa muda. Hakuna mtu aliyemuelekezea bunduki kichwani mwake; ulikuwa ni uamuzi wake wa hiari. Si yeye tu, wapo watu wengi ambao wakiwa na matatizo husema, "Ngoja nikanywe pombe nipoteze mawazo" bila kujua kwamba ulevi ukiondoka tatizo hilo itaendelea kubaki pale pale bila ufumbuzi tena utakuwa umeongeza jingine kwa fedha ulizotumia.
John alijikuta akiwa mtumwa wa ngono kwa njia hiyo hiyo. Kushindwa, ghadhabu, hatia, upweke - mawazo yoyote yasiyoleta faraja - aliamini yangeweza kuondoka kwa kufanya vitendo vya ngono. Alichagua kufanya vitendo hivyo vya ngono kama tiba yake. Uchaguzi siyo maradhi hata hivyo, ni uamuzi kati ya chaguzi mbili. John alichagua kujiingiza kwenye ngono badala ya kukabiliana na maisha halisi. Hakuna mtu anayeweza kupata raha halisi kutoka kwenye uraibu. Atapata masahibu kama ya John: faraja ipatikanayo ni ya muda mfupi sana.
Kuna hatua tatu za mtu kuingia kwenye uraibu: Katika hatua ya mwanzo kabisa, mhusika huwa anaamini kabisa kwamba uraibu wake unampa raha na faraja ya pekee; Katika hatua ya kati, mhusika huanza kujiuliza kama uraibu huo ni mzuri au mbaya, yaani unaleta raha inayotakiwa ama la, na; Katika hatua ya mwisho, mhusika hutambua kwamba uraibu huo husababisha maumivu kuliko raha, akini bado ataendelea kushikiliwa na utumwa huo.
Emile, mke wa John aliwahi kumuuliza mshauri, "John anafahamu kwamba hakupaswa kuanza vitendo vyake hivyo. Kwa nini anaendelea kuvifanya? Kwa nini asikome?"
Kama umeraibiwa, nina imani umeshawahi kujiuliza mwenyewe swali hilo mara nyingi sana. Jibu lake ni kwamba: Kama kukabiliana na uraibu hakukufanywa kwa usahihi, hakika utaendelea kuwa mtumwa kwa maisha yako yote, hata kama unajua kwamba tabia hiyo ni hatari. Watu hawajioni kama hawana matumaini katika kukabiliana na uraibu mpaka pale watakaposhindwa kuziacha tabia zao. Kama unajiona kwamba huna matumaini, hebu tutumie kushindwa kwako kama njia nzuri ya kujifunza. Tazama historia yako ya nyuma utagundua kwamba ulishindwa kukabiliana na uraibu wako kwa sababu utaratibu ulioutumia uliegemea katika kujirudia kwa tatizo. Watu wengi hawatambui kwamba wanayarudia matatizo yao, na ninadhani hata wewe hujui.
Utakuta mtu amefumaniwa na mke au mumewe aifanya mapenzi na mtu mwingine, au akipiga punyeto, au akitazama picha na mikanda ya ngono, badala ya kusema tabia hii sasa basi, na uiacha kabisa kama alivyoahidi wakati alipofumaniwa, siku chache baaaye atarejea vitendo hivyo hivyo!
Kama wewe si mtumwa, na una wasiwasi wa ukweli wa mwenzi wako katika kutaka kuacha tabia yake, muulize maswai yafuatayo: "Kama utapata njia halisi na ya kweli katika kuachana na tatizo lako, unaweza kuitumia?" "Kama utatakiwa kufanya kazi kwa bidii, na hiyo ikawa rahisi zaidi kuwa huru kutokana na uraibu wako, unaweza kufanya hivyo?" Kama mpenzi wako atajibu "ndiyo" katika masali yote, usikate tamaa. Mungu anamsaidia yule anayejisaidia!
Ngano za uraibu
Tunaishi katika ulimwengu uliogubikwa na vyombo vya habari. Utapagawisha sana na mawazo ya uraibu kwa muda mrefu sana, unachotakiwa kufanya ni kuwa makini ili kwamba harakati zako za kupambana na uraibu wa ngono zisiharibiwe na mambo mengine. Hebu ngoja tujadili baadhi ya yale yaliyo maarufu: Hakuna kitu kinachoitwa uraibu chanya kwa sababu uraibu wote unabomoa.
Ngano: Baadhi ya vitu husababisha uraibu: Hii kwa hakika ndiyo ngano kubwa kuliko zote. Kwa ujumla, utumiaji wako wa kitu fulani 'unaweza'  kukufanya ukawa mtumwa. Kwa mfano; Baada ya kufanyiwa upasuaji wagonjwa wengi huwa wanaruhusiwa kutumia dawa aina ya morphine. Morphine iko katika mfumo wa heroin, na ina nguvu sana. Lakini watu wengi ambao wanatumia dawa ya morphine baada ya upasuaji huwa siyo waraibu. Makumi kwa mamilioni ya watu wanavuta bangi. Wewe unaweza kuwa mmoja wao. Lakini wapo wachache ambao huitumia katika kiwango ambacho huwadhuru, unakuwa uraibu. Watu wengi wameshawahi kunywa pombe, wewe unaweza kuwa mmoja wao, lakini wachache ndio hugeuka kuwa 'walevi-mbwa'. Mamilioni ya watu wameshawahi kutumia cocaine, crack na dawa nyingine za kulevya.
Tofauti baina ya mtu aliyeathiriwa na asiyeathiriwa haihusiani na kitu hicho. Tofauti ipo katika uchaguzi wa kila mmoja kuhusu matumizi ya kitu chenyewe. Angalia maisha yako. Ulifanya uchaguzi katika matumizi mabaya ya vitu. Vitu haviwezi vikakuleteza ukafanya vitendo vya uraibu kuliko: Vitabu vinakufanya wewe usome; Gari zinakufanya wewe uendeshe; Mai yanakufanya uwe na kiu.
Ngano: Uraibu ni kushindwa kiroho: Maadili na uraibu ni vitu viwili tofauti. Kwa mfano, kumnyanyasa mtoto ni suala la kimaadili na kiroho kuliko uraibu. Mtu mwenye uraibu wa kula sana hana tatizo la kiroho, bali ni tatizo kama matatizo mengine.
Ngano: Uraibu unarithiwa: Baadhi ya "wanazuoni" wanaai kwamba kuna jeni (genes) fulani ya ulevi ambayo huwafanya watu kuwa walevi wa maisha, tena jeni hizi zinaweza kurithishwa kwa vizazi vyao. Ukweli unaonyesha kwamba huu ni uongo wa mchana kweupe. Wapo mamilioni ya watu ambao wazazi wao ni ni walevi wa kupindukia lakini wao hawajawahi hata kuonja kileo au dawa za kulevya maishani mwao. Wapo mamilioni ya watu ambao ni walevi mbwa na watumiaji wa awa za kulevya (mateja) lakini wzzi wao hawajawahi uvigusa vitu hivyo. Hii ni hekaya tu ambayo haina maana yoyote ile na kama utaisikia huko mitaani ipinge kwa nguvu zote.
Ngano: Uraibu unasababishwa na matangazo ya ajabu na hatari. Kwa mfano: Matangazo ya pombe na sigara huwaanya watu walewe na wavute sigara. Mitandao ya ngono na majarida ya ngono huwafanya watu wawe wazinzi. Filamu zinawafanya watu watumie dawa za kulevya.
Malumbano haya yanakufanya ujione kwamba wewe huna uamuzi wa hiari, kwamba wewe ni matokeo ya soko la vyombo vya habari. Lakini siyo kweli hata kidogo. Hebu ngoja tuangalie mambo machache: Makumi kwa mamilioni ya watu walikuwa wameathirika na uvutaji wa sigara na ulevi katika uliokuwa Umoja wa Kisovieti (USSR) na wakati huo hakukuwa na matangazo yaliyoruhusiwa, yaani serikali ilikuwa imepiga marufuku matangazo wakati huo wa Ujamaa na Kujitegemea.
Wapo mamilioni ya watu walioathirika na tabina na vitendo vya ngono ingawa huwa hawatazami picha za ngono. Wanapenda kitu hlisi au wanatumia fikra zao tu. Matumizi ya dawa za kulevya yalikuwa yamesambaa hata kabla Hollywood haijaanza kuonyesha athari za matumizi hayo. Uraibu hausababishwi na sehemu ya soko; unatokana na uchaguzi wa mtu anayetaka kuyakimbia maisha halisi na kwenda katika maisha ya kufikirika.
Kwa kuwa tumeziona hekaya hizi, sasa na tuangalie dalili halisi za utumwa wa ngono.
 
Dalili za Utumwa
Dalili: Tabia huongezeka wakati muda ukisonga mbele
Mtu huanza kujihusisha na utumwa kwa kutumia kitu au shughuli fulani kuyakimbia masumbufu ya maisha. Kukimbia huku hushindikana kwa sababu utoro huwa haufanikiwi - na mara zote huharibu matatizo ya maisha. Kisha - na hili ndilo kosa kubwa zaidi - mtu huyu huamua kujikita zaidi kwenye utumwa huu badala ya kupambana n tatizo linalomfanya atoroke.
Mzunguko huu wa utoro-kushindwa-utoro zaidi ndio husababisha tabia za uraibu kuongezeka kila wakati. Haihusiani chochote na mlingano wa kikemikali au mazingira. Mhusika huamua kuchagua kutoroka hata kama majiribio ya utoro siku zote hushindikana. Hatimaye, baada ya muda, waathirika wote hufikia kiwango cha utumwa uliokithiri na hakiongezeki; hubaki hapo hapo tu.
Jinsi ya kumsaidia mwathirika
Baadhi ya watu walioathirika hujaribu kukana matatizo yao kama alivyofanya William, mtu wa makamo na mmoja wa watu waliokuwa wakipewa ushauri naaha na rafiki yangu Joe. Yeye alisema: "Sijaongeza tabia zangu za uraibu kwa miaka 10, kwa hiyo sina uraibu."
Kama unataka kumsaidia ama kumfahamu mtu kama William, muulize swali hili: "Tabia yako imewahi kupungua katika miaka michache ya kwanza?" Kwa vyovyote vile atajibu "Ndiyo." Mara mtu wa aina hiyo atakaposema kwamba tabia yale imepungua au haijaongezeka, usiende mbali sana. Badala yake, angalia dalili nyingine, kwa sababu tabia nyingine hupungua kulingana na muda pia. Mtu aliyeathirika kutokana na tabia yake ya kujichua, kama William, hawezi kupiga punyeto kila mara katika umri wa miaka 35 ya sasa kama alivyokuwa na umri wa miaka 19. Wanaokula kupita kiasi hupunguza kasi yao kadiri wanavyokua, lakini bado wataendelea kutumia chakula zaidi. Katika hatua ya mwisho, walevi wengi hunywa kidogo lakini bado watakunywa katika mtindo ule ule wa utumwa. Kama tabia inaendelea kadiri muda unavyosonga mbele ni dalili tu, siyo uthibitisho wa mwisho. Ni kidokezo kikubwa kama kitachanganywa na matatizo mengine.
Dalili: Tabia inambomoa mtu binafsi
Uraibu unaegemea zaidi katika matumizi mabaya ya kitu au vitendo vibaya. Matumizi mabaya ya kitu chochote kile au kitendo chochote kibaya huleteleza matatizo makubwa zaidi.
Jinsi ya kumkabili mwathirika
Baadhi ya wathirika wa uraibu huwa wanasema, "Simuumizi mtu yeyote; mimi napata raha isiyo na madhara." Inaweza kuwa kweli, kwamba kujichua kwako kunakupa raha bila kumuumiza mtu yeyote, lakini hebu fikiria kama una mke au mpenzi na wewe ukaendelea na vitendo vyako hivyo, je, unaweza kumpatia mapenzi ya kweli na ya dhati? Unaweza kuyafurahia mapenzi halisi na yale ya kufikirika uliyoyazoea? Kifupi hapana, kwa sababu wataalamu wanasema kwamba, kama mtu ameshazoea kujichua basi akikutana na mwanamke au mwanaume halisi uwezo wake wa kufanya mapenzi huwa mdogo na mara afikiapo mshindo huchoka na kukosa raha ya kuendelea na tendo hilo. Aidha, ili afikie mshindo, huwa na kawaida ya kufikiria ni wakati gani mzuri aliowahi kuufurahia katika vitendo vyake.
Kama unataka kumkabili mtu aliye na uraibu na anayekana kwamba vitendo vyake viko sahihi kwa sababu hamuumizi mtu, pitia mambo yaliyoko chini taratibu ukiwa naye. Usizitumia pointi hizi kwa ajili ya kumshambulia. Tazama orodha kama nafasi ya kuperuzi na kutambua ukweli wa mambo: Vitendo vya uraibu huchuku muda mrefu na kugharimu fedha nyingi; Waathirika wengi hawaelewi jinsi wanavyopoteza muda na fedha nyingi katika vitendo vyao. Wengine wanajua na kutegemea kwamba wanaweza kuacha vitendo hivyo vinavyowapotezea muda na fedha zao.
Kwa mtu mwenye uraibu: Kama hujui kiasi gani cha muda na fedha unachotumia kwenye uraibu wako, sasa ni wakati mzuri kunza kufikiria hilo.
Kwa mwenza wako: Kama unajaribu kumkabili mtu mwenye uraibu, mwambie akuandikie kwenye karatasi kila kitu anachotumia au kugharamia katika tbia hiyo na kuchunguza muda anaoutumia katika hilo. Mambo haya peke yake yanaweza akamshtua na kumfanya mwenzi wako akiri kuhusu uraibu wake.
Huharibu afya ya mwili wa mtu. Uraibu mara nyingi hufanyika mpaka kiwango cha kuchoshwa kwa mwili. Watu wengi wenye matatizo haya huwa hawaelewi uchovu mwingi wa mwili unaosababishwa na tabia za uraibu mpaka watakapoiacha tabia hiyo.
Kwa mtu mwenye uraibu: Wakati mwingine utakapojisikia kuchoka sana mwili, fikiria kuhusu mara ya mwisho ulipofanya vitendo vya uraibu. Ilichangia kutokana na uchovu huo? Ndicho kilikuwa chanzo kikubwa cha uchovu?
Kwa mwenza wako: Waathirika wengi wanaokana matatizo yao watapinga na kudai kwamba uraibu wao hupunguza msongo wa mawazo na kuwaongezea nguvu. Huu unaweza kuwa utetezi mgumu kuushinda. Hata hivyo, waathirika wote huwa wanachoka mara wanapomaliza vitendo vyao vya uraibu. Mulize mwenza wako, "Unajisikiaje mara unapomaliza kitendo chako (kama kujichua, kuvuta sigara, bangi, dawa za kulevya, kutazama picha za ngono, kuzini, n.k.)?" Inawezekana hicho ndicho kitu pekee unachokihitaji.
Kama atakataa kwamba huwa hafanyi vitendo hivyo, basi hii inaonyesha kwamba tatizo ni kubwa zaidi. Badala ya kumfanya akiri kuhusu uraibu wake, muulize, "Unataka kusema kwamba huwezi kuongeza nguvu na kukabiliana na msongo wa mawazo katika njia za kawaida? Haitakuwa vizuri kwako kutegemea fikra zako mwenyewe badala ya vitu vingine vya kufikirika, kula sana, kufanya ngono kwa lazima?" Hiyo inaweza kumsaidia kuelewa kwamba kweli yeye ni mtu tegemezi.
Dalili: Tabia hiyo huleta athari kwa wengine
Baadhi ya kadhia hizi zinaweza kuwa zimezoeleka miongoni mwa jamii yetu: Henry alivunja ahadi na marafiki, familia, na wafanyakazi wenzake kutokana na vitendo vya uraibu; Watoto wa Maria kwa bahati mbaya walijikuta wakimfumania mama yao akitazama mikanda ya video ya ngono usiku wa manane huku akiwa anajiingiza vidole sehemu za siri; Familia ya Eric ilikuwa inaishi kwa mlo wa kubahatisha kutokana na yeye kutumia fedha nyingi kwa makahaba na wanawake wengine; Badala ya ndoa ya upendo na mahaba ambayo Doreen aliitegemea, alikumbana na mateso makubwa kutoka kwa mumewe Damas ambaye aliweza kukaa miezi kadhaa bila kuanya naye tendo la ndoa, hali iliyomlzimisha dada huyo atafute bwana wa pembeni kukidhi haja zake za mwili; Sylvia alitekeseka sana moyoni kwa miaka mingi kwa sababu mumewe Jonathan alihusudu sana na kutumia muda mwingi katika kupiga punyeto na kutazama picha za ngono kuliko alivyofanya naye mapenzi; Sally hakufanya mapenzi kwa miaka mitano na hakuelewa kwamba hali hiyo ilitokana na uraibu wa ngono wa mumewe, yeye alifikiri kwamba tatizo liko kwake; Tatizo jingine la kutisha, Hamisi alipata ugonjwa wa zinaa kutokana na tabia ya uzinzi ya mumewe; Kwenda matembezini na mumewe yalikua kama mateso makubwa kwa Mwasiti kwa sababu mumewe Juma alikuwa akiwakodolea macho wanawake kana kwamba anataka kuwavua nguo; Hassan aliwanyanyasa sana akina dada waliokwenda kuomba kazi ofisini kwake na kukataa kufanya naye mapenzi kama moja kigezo cha kuajiriwa naye; n.k.
Kwa ujumla yapo mambo mengi sana ndani ya jamii yetu ambayo yanatokea siku hadi siku, na yote ukiyatazama utaona kwamba ni uraibu tu. Hivi sasa dunia imegubikwa na maradhi mabaya ya UKIMWI, na ukiangalia kwa undani watu wengi wanapata maradhi haya wakiwa nani ya ndoa, tena wameishi kwa miaka mingi sana. Sasa jiulize, wamepataje maradhi hayo kama siyo mmoja wao kutokuwa mwaminifu? Jibu nadhani kila mmoja wetu analo kichwani mwake, au siyo?
Katika matukio mengine, mtu anaweza kuonekana mnyama ndani ya jamii kwa utumwa wake wa ngono kiasi cha kubaka watoto kama Maumba alivyofanya, au kuhusudu kuchungulia watu wakifanya mapenzi kama Ally alivyofanya, au mpendna mashoga kama David afanyavyo. Lakini matatizo haya siyo mengi kama yale mengine.
Watu wengi wenye uraibu, kama ni wastaarabu na wanawajali wenzao na uhusiano wao, watakiri kuhusu madhara waliyowasababishia wengine. Kama unakabiliana na mwathirika ambaye hayuko tayari kukiri madhara aliyowasababishia wengine, usikae kimya na badala yake jitahidi mpaka akiri, lakini katika hili lazima ujindae na wakati mgumu zaidi. Unapaswa kukusanya taarifa zako pamoja kabla ya kumkabili. Angalia katika kila upenyo ambao mwenzi wako anaweza kuutumia. Ninaamini mpaka hapa unajua mambo ya msingi unayopaswa kumweleza. Tazama namna ambavyo wewe utakwenda kuitikia, kama utashindwa kuja na maelezo yanayofaa, basi mweleze, "Sawa, huu ndio ukweli wenyewe kuhusu matatizo yako. Siwezi kubishana na wewe kuhusu hili, unaweza kufanya au kuacha." Kwa watu ambao ni wagumu kukubali, nafasi pekee ambayo unaweza kuitumia ni kuwaambia, anya hivi au acha.
Dalili: Tabia hii hubadili hisia
Watu wanapotumia dawa za kulevya kwa ajili ya kujisikia vizuri (wengine hujiona kama wanaelea angani) au wanapokunywa pombe kwa minajiri ya kupoteza mawazo, wanajaribu kubadili hisia zinazowakera badala ya kukabiliana na tatizo husika. Wengine wanatumia dawa mbalimbali za hospitali, mapenzi, na ama kula sana katika namna ile ile ya kutoroka matatizo.
Watu walioathirika sana na tabia hii watakiri kwamba wanatumia tabia hii kubadili hisia zao. Lakini baadhi wanaweza kusema pia, "Kwani kuna ubaya gani?" Swali hili litakuwa na tafsiri za aina mbili kwa sababu mtu huyo anaweza kumaanisha: Kwani haifai kimaadili kubadili hisia zako? Na/au Kwani itaniumiza kama nitazigeuza hisia zangu?
Njia nzuri zaidi ya kujibu swali hilo "Kwani kuna ubaya gani?" ni, "Siyo vibaya kimaadili wala siyo dhambi kukiri. Ni kwamba haifai kwako. Hakika inaweza kukuumiza tabia hiyo. Mara nyingi ni vizuri kwako kukabiliana na hisia zako badala ya kuzikimbia."
Kuna baadhi ya waathirika ambao siyo rahisi kukiri kwamba wanakuwa na tabia hiyo kwa ajili ya kubadili hisia zao. Hili ni swali unalopaswa kuwauliza: "Kama wewe siyo mtumwa, basi kwa nini (unalewa, unakula kupita kiasi, unazini na kuhusudu ngono, nk.) kila unapokuwa na msongo wa mawazo, upweke, hati, hofu, kushindwa, kutwezwa au hisia nyingine zisizo njema?" Kama watakana, basi wakumbushe nyakati ambazo ulishawahi kuwaona wakiwa katika tabia hizo katika harakati zao za kutoroka kukabiliana na maisha halisi.
Dalili: Mwathirika hujaribu kuacha
Mkanganyiko, hatia, fadhaa, hofu, aibu, na mambo mengine huambatana na uraibu kwa sababu ni njia za asili za kumweleza mwathirika, "Kabiliana na tatizo lako au ukitaka endelea kujiona mnyonge mpaka ufanye matendo hayo." Katika hatua ya mwisho ya uraibu ambapo itaonekana kwamba uraibu lilikuwa ni kosa kubwa sana, waathirika wengi hutumia sehemu kubwa ya maisha yao yaliyosalia: Kujaribu kuacha; au, Kudhani kwamba wanaweza kuacha; au Kujiandaa kwa jaribio lao linalofuata la kuacha.
Nini cha pekee kuhusu utumwa wa ngono?
Hatukuzaliwa na tamaa za asili za kulewa pombe, kutumia uraibu wa dawa za kulevya na mihadarati au kuharibu fikara zetu na matibabu ya dawa za hospitali. Tumezaliwa na tamaa njema za asili kuhusu mapenzi, kazi na chakula.
Uraibu ambao shina lake ni msukumo wa kiasili unapaswa kutibiwa tofauti n uraibu unaotokana na mambo yasiyo rasmi. Sababu zake ni hizi: Msukumo wa kiasili unapaswa kutekelezwa. Kama utajaribu kuliondoa tatizo la uraibu unaotokana na tamaa za asili, utakuwa unapambana na asili. Kuishi maisha bila ya kufanya mapenzi wala kazi humfanya mtu achanganyikiwe, afadhaike na ahuzunike. Kama utaacha kula kabisa hakika utakufa. Na ingawa baadhi ya watu wanasema kwamba kuka bila kufanya mapenzi hakuna madhara, mimi napingana nao, kwa sababu watu wengi ambao wameamua kuishi maisha ya useja na ukapera wana matatizo mengi ya kisaikolojia.
Dalili 10 kwamba wewe ni mtumwa wa ngono
1. Unafanya mapenzi na zaidi ya mtu mmoja kwa mwezi.
2. Unajichua kila mara (mara 3 hadi 25 kwa wiki).
3. Unawageuza wapenzi wako kama chombo tu badala ya "kufanya nao mapenzi."
4. Una zaidi ya mikanda 10 ya video za ngono au majarida ya ngono nyumbani kwako.
5. Unafanya mapenzi ya kufikirika.
6. "Unazunguka," lakini unaweza kusema 'watu wanakutazama....'
7. Unafanya mapenzi katika sehemu za hatari.
8. Unaendelea kupigania "mapenzi makubwa"
9. Unafikiria na/ama kuzungumzia sana ngono.
10. Unadhani kwamba unaweza kuwa bingwa wa ngono.
 
Niandikie: brotherdannys5@gmail.com

No comments:

Post a Comment