Friday, 8 November 2013

CHEKA KIDOGO: KOPO LA CHOONI LAZUA MAMBO

Mchoro kwa hisani ya fas-digiclass.rutgers.edu

Jamaa mmoja aliamua kufanya kile ambacho hakikutarajiwa na wengi. Kila siku akishikwa na haja kubwa alijaza maji kwenye kopo na kwenda nalo chooni.
Baada ya kumaliza haja alipoangalia akakuta maji yote yamekwisha kabla hajayatumia, akadhani ni muujiza. Lakini hakutawadha. Siku ya pili hivyo hivyo.
Sasa siku ya tatu akaamua kulichunguza kopo la miujiza na ndipo alipogundua kwamba kumbe lilikuwa limetoboka.
Kwa hiyo alipoingia chooni akaamua kutawadha kwanza kabla ya kujisaidia.
Alipomaliza akatoka mbio na kusema: “Nimeliweza leo, halafu ndo nikajisaidia.”

No comments:

Post a Comment