Saturday, 16 November 2013

NITAWASUBIRI POLISI!

Mwanamke na mwanamume walipata ajali. Magari yao yaliharibika vibaya, lakini kwa mshangao hakuna kati yao aliyeumia.
Baada ya kutoka nje ya magari yao, mwanamke akasema: "Duh, hebu angalia magari yetu - hakuna kilichosalia! Hii itakuwa dalili ya Yeye (Mungu) kwamba tunatakiwa kuwa marafiki na tusilaumiane kwa kosa lolote."
Mwanamume akajibu: "Kweli kabisa, nakubaliana na wewe moja kwa moja."
Mwanamke akaonyesha chupa ya wine iliyokuwa imedondoka chini na kusema: "Walau chupa hii ya wine kutoka kwenye siti ya nyuma ya gari langu haikuvunjika. Hakika Mungu anataka sisi tunywe wine hii na tusherehekee bahati yetu ya kunusurika na ajali."
Akampatia mwanamume chupa hiyo ya mvinyo. Mwanamume akaitikia kwa kutikisa kichwa, akaifungua na kugugumia katika theluthi ya mvinyo ili kupoza fadhaa zake. Mwanamke akachukua chupa hiyo, akaifunga na kumrudishia tena.
Mwanamume akauliza: "Hunywi kidogo?"
Mwanamke akajibu: "Hapana. Nadhani nitawasubiri polisi."

No comments:

Post a Comment